Burudani

Mc Pilipili alazwa hospitali ya Bugando, baada ya kupata ajali

By  | Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili amepokewa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea ajali hiyo, na amesema Mc Pilipili alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya Mondo mkoani humo na katika gari hilo kulikuwa na mtu mmoja ambaye naye amepata majereha.

Kwa upande wa Katibu wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga amesema wamepokea taarifa za ajali hiyo siku ya leo (jana).

Maswenga amesema Mc Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi wikiendi iliyopita na alikuwa akisafiri kuelekea Mwanza, Maswenga ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa za ajali hiyo wamekuwa wakiwapigia simu ila jitihada  zao zimengonga mwamba hivyo hawapatikani hewani.

Naye Afisa uhusiano wa hospitali ya Bugando, Lucy Joseph amethibitisha kupokewa Mc Pilipili na amesema taarifa zaidi kuhusu hali yake zitatolewa baadaye.

Chanzo: Mwananchi

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments