Habari

Mch. Msigwa na Mnyika wajilipua Dodoma, waitaka ripoti ya CAG bungeni na kuhoji CCM kung’oa bendera za upinzani (+video)

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amehoji kwanini bendera za vyama vya upinzani zinang’olewa kwa nguvu na kuwekwa za CCM kwenye maeneo yote ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapopita kwenye ziara yake kikazi.

Msigwa aliuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu mapema leo Aprili 12, 2019 bungeni jijini Dodoma.

Kwa upande mwingine, Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. John Mnyika amehoji ni kwanini Wabunge hawajagawiwa ripoti  mpya ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama kanuni za Bunge zinavyosema.

Mnyika ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 12, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika Utawala Bora, ambapo amesema kwamba kitendo cha wabunge kutogawiwa ripoti hiyo hakiwezi kuungwa mkono na wabunge kwa kuwa kinakiuka kanuni za Bunge.

Hata hivyo, ombi hilo la Mnyika limegonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusema ripoti hizo za CAG haziwezi kugawiwa kwa wabunge kama Mnyika anavyotaka kwa kuwa kanuni haziruhusu kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents