Burudani

Mchekeshaji Kathy ampigia magoti Donald Trump

Mchekeshaji wa Marekani, Kathy Griffin ameomba msamaha kutokana na picha aliyopiga akiwa ameshika kichwa cha rais wa nchi hiyo Donald Trump kikiwa kimekatwa huku damu zikitoka.

Kupitia mtandao wa Twitter, Kathy ameweka video yake akiomba radhi huku akisema, “I moved the line, and then I crossed it. I went way too far. The image is too disturbing. I understand how it offends people.”

Kathy ameongeza kwa kusema kuwa tayari amemwambia Tyler Shields ambaye alimpiga picha hizo kuzifuta haraka.

Picha hizo zimezua mjadala mkubwa mitandaoni. Mchekeshaji huyo ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya uigizaji za Emmy amekuwa akipinga sera za utawala wa Trump.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents