Burudani

Mchepuko wamponza rapper Rick Ross

Rick Ross aingia katika kesi nzito ya kuchepuka.

Rapper huyo anadaiwa kumsaliti mpenzi wake Liz Hagelthorn na kumpatia ujauzito mwanamitindo Briana Camille.

Tetesi hizo zimeibuka baada ya MediaTakeOut kumpongeza mchepuko huo wa Rick Ross kupitia katika moja ya picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram na kuandika, “Congrats to you and Rick Ross.”

Kama ni kweli ujauzito huo ni wa rapper huyo, basi atakuwa ni mtoto wake wa tatu baada ya Toie Roberts na William Roberts ambao alizaa na wanawake wawili tofauti. Tetesi hizo zinaweza zikawa mbaya katika mahusiano ya Ross na mpenzi wake Liz Hagelthorn ambao wanatarajia kufunga ndoa muda si mrefu.

Hizi hapa chini ni baadhi ya picha za Briana Camille akiwa na ujauzito unaodaiwa ni wa Rick Ross.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents