Bongo Movie

Mcheza Filamu John Stephano Maganga Azikwa Leo

Wacheza Filamu wakibeba jeneza la marehemu John Stephano Maganga.

Aliyekuwa mcheza filamu anayechipukia, katika tasnia ya filamu Tanzania, Marehemu John Stephano Magana ambaye alifariki dunia siku ya Jumamosi katika hospitali ya Taifa Muhimbil kwa tatizo la utumbo kujaa maji amezikwa leo, katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar-Es-Salaam.
Safari nzima ya mwisho kwa marehemu Maganga ilianza majira ya mchana ambapo alifikishwa nyumbani kwao Mwananyamala majira ya saa saba mchana ambapo shughuli ya kumuga ilichukua takriban masaa mawili.
Katika msiba huo ambao ulihudhriwa na wengi kati ya wasanii wenzake kulikuwepo Baba Mzazi, Mdogo wake wa kike, Mama Mdogo, Mashemeji ndugu jamaa, wadau na marafiki wakiongozwa na Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Bwana Mwakifamba Simon.
Aidha mama mzazi wa marehemu hakuwepo nchini lakini alitoa ujumbe wake kupitia njia ya simu katika makaburi ya kinondoni wakati wa kutoa salamu za pole kwa ndugu Jamaa na Marafiki pamoja na wadau wa tasnia ya filamu.
Mungu Ailaze Pema peponi roho ya marehemu John Stephano Maganga.
Angalia

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents