Burudani

Mcheza kikapu na mume wa zamani wa mdogo wake Kim Kardashian yupo hoi na hajitambui kwa kuzidisha dawa za kulevya

Mchezaji wa kikapu wa Marekani, Lamar Odom anapigania maisha yake baada ya kudaiwa kutumia kiasi kikubwa cha cocaine kiasi cha kupatwa na kiharusi na figo zake kushindwa kufanya kazi.

lamar-odom-and-khloe-kardashian

Lamar ni mume wa zamani wa mdogo wake na Kim Kardashian, Khloe.

Kufuatia habari za mchezaji huyo wa zamani wa LA Laker kuzidisha madawa ya kulevya, Khloe alienda haraka kwenye hospitali ya Sunrise ya jijini Las Vegas kumuona.

Muda mfupi alifuatwa na dada zake Kim Kardashian West na mama yao Kris Jenner. Madaktari walidai kukuta kila aina ya madawa ya kila aina kwenye mfumo wake wa damu.

Kwa sasa Odom anatumia mashine ya kumsaidia kuishi huku moyo wake, mapafu na figo zikishindwa kufanya kazi.

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa Odom aliamua kubwia unga kwa kiasi kikubwa baada ya kupokea simu iliyomuudhi inayohusiana uhusika wake kwenye show ya Keeping up with the Kardashians.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents