Michezo

Mchezaji ajipongeza kwa kunywa pombe uwanjani baada ya kutupia bao la umbali mrefu (+video)

Kiungo wa klabu ya Hammarby IF inayoshiriki ligi kuu Sweden, Kennedy Bakircioglu amefanya kitu kisicho cha kawaida baada ya kunywa kilevi ndani ya uwanja wakati akisherehekea goli lake alilofunga umbali wa mita 30.

Kennedy mwenye umri wa miaka 37 aliyeingia uwanjani akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Jappe Andersen dakika ya 73 amefanya tukio hilo baada ya kutupia bao la umbali huo mrefu.

The 37-year-old had been on the pitch for six minutes but caught a beer from a fan and drank it

Mchezaji huyo alitupiwa chupa ya bia na shabiki ndani ya uwanja wakati akisherehekea bao hilo na kuamua kuinywa pasipo jali kitu chochote.

Katika mchezo huo, Kennedy ametupia bao la tatu dakika ya 79, baada ya Jiloan Hamad na Bjoern Paulsen kuanza kufungua mlango wa mabao klabu ya Hammarby ambayo imeibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 0 dhidi ya IFK Goteborg mechi iliyopigwa hapo jana siku ya Jumatatu.

Kennedy Bakircioglu netted a stunning free-kick before finishing with a unique celebration

Kwa matokeo hayo imeifanya klabu ya Hammarby kushika nafasi tatu kwakuwa na pointi 47 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku yapili ikishikiliwa na Norrkoping wenye alama 49 na yakwanza ikishikiliwa na timu ya AIK wenye 57.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents