Michezo

Mchezaji aliyetua Simba amtesa Kaseja

 

Shija Mkina amemtesa kipa wa Simba Juma Kaseja katika mazoezi ya timu ya Simba yanayofanyika  kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Shija aliesajiliwa na Simba kutoka Kagera Sugar alifunga mabao manne maridadi Kaseja katika mazoezi ya juzi alhamisi yaliyokuwa chini ya kocha mkuu msaidizi Syller Said Mzirai.

Mkina ambaye ana uwezo wa kucheza hata nafasi ya kiungo pamoja na ushambuliaji alionekana kufanya vizuri katika mazoezi hayo na hata kutishia nafasi za nyota wa timu hiyo Mussa Hassan Mgosi na Emmanuel Okwi.

Habari nzuri kwa Mkina ni kuwa Mgosi atakuwa nje ya uwanja kwa siku tano hivyo kumpa nafasi kuzidi kutamba mazoezini.

Mgosi atakuwa akitibiwa Hospitali ya Aga Khan kwa muda wa siku tano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents