Michezo

Mchezaji Humoud aliyetimuliwa KMC kisa kutongoza wake wa wachazaji wenzake afunguka

Mchezaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga KMC Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ (31) amesema klabu yake hiyo imemtengenezea shutuma.

Gaucho ambaye aliipandisha daraja timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) alisema viongozi wa wa timu hiyo wanaongea maneno ambayo si ya kweli na walichopanga ni kumchafulia taswira yake bora ambayo imeitafuta kwa jasho zaidi ya miaka kumi.

Anasema mimi nilivunja mkataba na klabu ya KMC mwezi mmoja na nusu na kilichonifanya kuvunja ni kutokakana sikuwa napata nafasi ya kucheza bila ya sababu ya msingi tangu mwalimu mpya alivyofika.

“Niliandika barua ya kuomba kuachwa baada ya kushauriana na watu zangu wa karibu lakini nilipata majibu ambayo hayakuwa mazuri kutoka kwa viongozi wangu,” alisema.

“Majibu ambayo walinipatia natakiwa kurudisha vifaa vya timu na baada ya muda watakaa na wanasheria wao ili niwalipe ambavyo natakiwa kufanya hivyo jambo ambalo nalishangaa wakati mimi niliandika barua ya kuomba ambayo walikuwa na uwezo wa kunikatalia na kukubali kutokana na kuomba kwangu.

“Nimekaa zaidi ya muda mrefu nikiendelea kutafakali hilo nikiwa nje ya nchi nikiwa njiani narudi ndio nakutana na shtuma hizo za uzushi ambazo uongozi wa KMC imenitengenezea, ” alisema.

“Kama mtu ambaye jamii inanitambua nimeamua kuweka wazi kuwa hizo ni shtuma ambazo nimetengenezewa lakini hakuna ukweli wowote kati ya hayo mambo ambayo nimeambiwa nimefanya au kuhusika na uongozi wa KMC, ” alisema.

Uongozi wa KMC kupitia Mtendaji wake Walter Harrison ulisema hawakuwa na chaguo lingine zaidi ya kuachana na kiungo huyo kutokana na mambo ya utovu wa nidhamu ambao ilikuwa akifanya ndani ya timu.

“Tukio la kwanza kwa Gaucho lilijitokeza kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ambapo hakuanza kwenye kikosi cha kwanza, kocha alipohitaji kumtumia alisema ameacha vifaa vyake Dar.

“Siku chache baadaye yakatokea mengine, Gaucho alichukua simu ya mwenzake ambaye anakaa naye chumba kimoja na kuchukua namba ya msichana wa mwezake,” alinukuliwa Walter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents