Tupo Nawe

Mchezaji wa Ajax aliyepoteza fahamu miaka 2 iliyopita azinduka leo, Kaka yake athibitisha – Video

Mchezaji wa Ajax aliyepoteza fahamu miaka 2 iliyopita azinduka leo, Kaka yake athibitisha - Video

Baada ya miaka miwili, miezi nane na siku 19, mchezaji Abdelhak Nouri wa klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi ameamka kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza fahamu.

Mchezaji Abdelhak Nouri

Abdelhak Nouri mwenye umri wa miaka 22 hivi sasa, alipoteza fahamu katika mchezo wa kirafiki  dhidi ya Werder Bremen Julai 8, 2017, ambapo kwa mujibu wa familia yake, hivi sasa anahudumiwa akiwa nyumbani baada ya kuathirika katika ubongo.

Hivi sasa anaweza kula na kutazama mechi za soka akiwa amekaa katika kiti maalum, ikiwa ni hatua kubwa katika kuimarika kwa afya yake ikilinganishwa na hapo awali.

Kaka yake ambaye anamhudumia wakati wote nyumbani, amesema, “hajakuwepo nyumbani kwa muda mrefu, tunaangalia kwa ukaribu afya yake hapa. Hivi sasa anaweza kukaa, anafahamu kuwa yupo mahali gani, analala, anakohoa na anakula pia, bado anaendelea kuimarika akiwa anatutegemea“,.

Abdelhak amecheza jumla ya mechi tisa za kikosi cha kwanza cha Ajax kabla ya kipaji chake kukatishwa katika tukio hilo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW