Mchezaji wa NBA Jason Collins atangaza kuwa ni shoga

Mchezaji wa kikapu katika ligi ya mchezo huo nchini Marekani, NBA, Jason Collins ametangaza wazi kuwa ni shoga. Collins aliyezichezea timu za Washington Wizards na Boston Celtics hivi karibuni anakuwa mchezaji wa kwanza kwenye timu kubwa ya ligi hiyo kujitangaza.
jason_collins

Ameweka wazi kuhusu suala hilo zito kwenye makala moja ya jarida la Sports Illustrated inayoanza kwa kusema: I’m a 34 year old NBA center. I’m black . And I’m gay”.

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ni miongoni mwa watu waliotuma ujumbe wa kumuunga mkono mchezaji huyo.

Collins ambaye ni free agent katika mchezo huo wa kulipwa na aliyecheza misimu 11 ya NBA akiwa na timu sita, amesema alijaribu kupoteza hisia hizo kwa kuwa na uhusiano na wanawake lakini hakufanikiwa.

Mchezaji wa zamani wa ligi hiyo, John Amaechi aliwahi kujitangaza kuwa ni shoga lakini alikuwa amestaafu tayari.

Chanzo cha habari ni mahojiano aliofanya na jarida la Sports Illustrated http://m.si.com/2854664/an-nba-player-comes-out/

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW