DStv Inogilee!

Mchezaji wa Saint-Etienne auawa kwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyekuwa beki wa klabu ya Saint-Etienne inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, William Gomis amefariki dunia usiku wa jana kwa kushambuliwa na risasi.

Duru za habari zinaeleza kuwa, Gomes mwenye umri wa miaka 19 ameshambuliwa na bunduki aina ya AK47 katika mitaa ya La Seyne-sur-Mer.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa kijana wa miaka 14 amefariki dunia katika tukio hilo huku jeshi la polisi likiwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo ya Kalashnikov (AK47).

Mmoja wa makaka wa kijana Gomis pia aliripotiwa kufa kwa kushambuliwa na risasi wiki chache tu zilizo pita huku klabu ya Saint-Etienne ikithibitisha tukio hilo la mchezaji wao hii leo siku ya Jumatatu..

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW