Michezo

Mchezaji wa Simba, Pascal Wawa afananishwa na nyota huyu barani Ulaya 

Kunamsemo wa Kiswahili ambao umezoeleka sana unaosema duniani watu wawili wawili basi hivyo ndivyo wa wachezaji hawa wawili ambao huwenda hata hawafahamiani lakini picha zao zinaangaziwa zaidi kuwa ni watu ambao wanafana kwa muonekano wao.

Beki wa timu wa Simba, Pascal Wawa

Wachezaji hao ni beki wa timu wa Simba, Pascal Wawa na kiungo wa FC Barcelona, Arturo Vidal hawa wote wakiwa wamesajili mwaka huu kwenye klabu zao wanazozitumikia.

Kiungo wa FC Barcelona, Arturo Vidal

Katika muonekano wa kawaida Wawa na Vidal wanafana hasa katika mtindo wao wa nywele ambao wote wamenyoa nywele zao za pembeni na kubakiza kidogo katikati ya kichwa ambazo zinaelekea nyuma kichogoni.

Lakini pia wawili hao hufanana hata maumbile yao, kwakuwa na maumbile makubwa na yaliyo shiba hasa kiasi kwamba wanapokutana na wachezaji wenye miili midogo lazima kujidhatiti kukabiliana nao.

Kila mmoja ni mpenzi wa kujichora mwilini ‘Tattoo’ kwani ukiwaangalia mwilini mwao wote wamejichora kiasi kwamba kuwa na mfanano zaidi.

Picha za Pascal Wawa na Arturo Vidal zikiwa zimeunganishwa

Licha kufanana huko zipo pia tofauti za wachezaji hawa wawili ambao kila mmoja anaumaarufu kutokana na ligi anayoshiriki.

Pascal Wawa raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 32 anaitumikia Simba nafasi ya beki huku usajili wake ukiwa ni wa miaka miwili. Wawa ambaye alitangazwa kusajiliwa ndani ya timu hiyo Juni 28 mwaka huu aliwahi kuitumikia klabu ya Azam FC.

Wakati kwa upande wa Arturo Vidal  raia wa Chile mwenye umri wa miaka 31 anayeitumikia miamba ya soka ya Hispania FC Barcelona nafasi ya kiungo ametuwa hapo rasmi Agosti 6, 2018 kwa dau la pauni milioni 32, akitokea Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents