Shinda na SIM Account

Mchezaji wa timu ya Al Ittihad avunjiwa mkataba baada ya kugundulika ana maambukizi ya HIV

Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad, inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, amevunjiwa mkataba wake, baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo ana maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Nlend

Jarida la KingFut limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwenye vyombo vya habari.

Mshambuliaji huyo ambaye ameitumikia timu ya Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.

Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August.

Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW