Michezo

Mchezaji wa timu ya taifa ya Denmark atembelea kwao Tanga

Mchezaji wa klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Denmark, Yussuf Poulsen amewasili nchini Tanzania  na kutembelea Mkoani Tanga, ambapo ndio asili ya baba yake alipotokea.

Mchezaji wa kimataifa wa Denmark na klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi ya Ujerumani (Bundesliga),Yussuf Poulsen (kulia)

Poulsen raia wa Denmark, ambapo ndiyo kwenye asili ya mama yake,  lakini baba yake ambaye alishafariki ni mwenye asili ya kabila la mdigo.

Huyu ni mchezaji anayekipiga kwenye timu inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Ujerumani (Bundesliga) katika  klabu ya RB Leipzig.

Baba wa mchezaji huyo alifariki kutokana na maradhi ya kansa wakati Poulsen akiwa na umri wa miaka sita, kwa sasa Yussuf Poulsen yupo jijini Tanga, na ameweza  kutembelea familia ya upande wa baba yake.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents