Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mchezaji wa Uingereza aondoka Urusi kukiwahi kichanga nyumbani

Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza, Fabian Delph ameachana na kikosi cha meneja Gareth Southgate kilichopo nchini Urusi kwaajili ya kuwahi kumuona mkewe anavyojifungua.

Delph ambaye ni kiungo wa klabu ya Manchester City amefanya maamuzi hayo mapema wiki hii wakati Uingereza ikielekea kwenye mchezo wake wa 16 bora dhidi ya Colombia siku ya Jumanne hali iliyopelekea kukosekana kwenye mechi hiyo.

The midfielder tweeted a picture of his special reading material for the flight back to Russia

Kiungo huyo ameposti picha akionyesha kuwa yupo njiani akirejea Urusi. 

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amefanikiwa kumshudia mkewe akijifungua salama mtoto wao wa tatu hapo jana asubuhi siku ya Jumatano na sasa akiwa safarini kurejea kwenye kikosi chake cha Uingereza kilichopo kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Fabian Delph poses with wife, Natalie (right), before the birth of their third daughter

Fabian Delph akiwa na Mke wake, Natalie (kulia), kabla ya kujifungua mtoto wao wa tatu

Uingereza ilifanikiwa kuifunga Colombia kwenye hatua ya 16 bora  na sasa ikitarajiwa kukabiliana na timu ya taifa ya Sweden hatua ya robo fainali.

Delph featured against Panama and Belgium before making the trip back to England last week

Delph dhidi ya Panama na Ubelgiji kabla ya kurejea Uingereza

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW