Michezo

Mchezaji wa zamani wa Newcastle afariki dunia

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United na timu ya taifa Ivory Coast, Cheick Tiote amefariki dunia wakati wa mazoezi nchini China.

Tiote mwenye miaka 30, ambaye alikuwa akichezea timu ya Beijing Enterprises inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.

Kwa mujibuwa wakala wa mchezaji huyo, amesema amefariki baada ya kuzimia uwanjani. “Ni huzuni kubwa, ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi,” amesema wakala huyo.

Tiote alianza kuwa mchezaji wa kulipwa nchini Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10.

Pia ameshawahi kuichezea timu ya Newcastle kwa misimu saba na mechi kucheza michezo 138. Tiote alizaliwa nchini Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.

Kupitia mtandao wa Twitter wa Newcastle wameandika, “We’ll never forget you, Cheick. ⚫️⚪️.”

Naye Papiss Cisse ambaye amewahi kucheza na Tiote wakiwa Newcastle, kupitia mtandao huo ameandika, “Goodnight brother, You will be missed. My heart goes out to his family. Gone too soon #RIPcheiktiote.”

Wakati huo huo Vicent Company wa Manchester City,naye ameandika, “I am speechless and so incredibly sad. Cheick Tioté was one of the nicest and toughest teammates I have ever had. Rest in peace brother.”

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents