Burudani

Mchezo huu hatari zaidi duniani waleta maafa nchini Hispania (picha+video)

Kama wewe ni mvivu wa kukimbia au pengine ni mzito kwenye mazoezi basi kwa mwezi huu una kila sababu ya kutalii mjini Pamplona nchini Hispania kwani bila shaka utarudi ukiwa mwepesi, hii ni kutokana na tamasha la namna yake la mchezo wa Running of the Bulls kufunguliwa rasmi.

None
Moja ya wanaume wakitimua mbio wakiyakimbia Mafahali yaliyojawa na gadhabu.

Mchezo wa Running of The Bulls kiufupi unahusisha Mafahali (Ng’ombe wa Kiume) sita hadi 10 wenye nguvu ambao huachiwa kwenye uwanja uliojaa watu na kisha kuanza kukimbizana.

Kitendo hicho cha kufunguliwa ng’ombe hao watu huanza kuwazonga na kisha kuanza kukimbizana na ng’ombe hao karibia siku nzima kuzunguuka mji husika.

Watu wote wanaohudhuria kwenye tamasha hilo wanaume kwa wanawake huvalia mavazi meupe au nguo nyekundu na kisha kuingia mtaani kuwazonga mafahali hao.

Habari mbaya ni kwamba kwa mwaka huu tayari mtu mmoja ameshafariki dunia kutokana na mchezo huo huku wengine Tisa wakijeruhiwa vibaya hapo jana Jumapili hii ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la AP.

Running The Bulls ni mchezo unaopendwa zaidi kwa nchi za Hispania, Ureno na Canada na kwa mwaka huu tamasha la mchezo huo limeanza Jumamosi Julai 07 na litamalizika Julai 14, 2018. Tazama video ya mchezo huo jinsi ulivyofana nchini Hispania ikiwa leo umeingia siku ya tatu tangu tamasha hilo lianze

https://youtu.be/56MMmNy1faM

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents