Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mchina atwaa taji la Miss World 2012

Mshindi wa shindano la urembo la Miss World ni Yu Wenxia kutoka nchini China. Ushindi huo umetangazwa muda sio mrefu jijini Ordos nchini Mongolia ambapo mshindi wa pili ametokea Sophie Elizabeth Moulds wa kutokea Wales na mshindi wa tatu akiwa Jessica Michelle Kahawaty wa Australia.

Yu Wenxia mwenye miaka 23,ni mwanafunzi wa muziki ambaye anadhamiria kufundisha muziki pia.

Washindi kutoka Africa waliopeta katika mashindao hayo ni warembo kutoka Kenya na South Sudan, ambapo Kenya alifanikiwa kutinga mpaka Nusu fainali za shindano huko mrembo kutoka South Sudan akifanikiwa kufikia hatua ya finali.

Tangu hatua za awali, mrembo wa South Sudan alionekana kushiriki na kufanikiwa katika michuano ya Beach Beauty, pamoja na shindano la Top Model.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW