EventsHabari

Mchina awa Miss World

Miss World 2007BAADA ya kuendesha shindano la urembo la dunia kwa mwaka wa nne, China hatimaye imemtoa mrembo katika shindano lililofanyika jana katika Ukumbi wa Hainan Province, China. Mrembo huyo, mwenye umbile la ulimwende wa kweli, Zi Lin Zhang alitangazwa jana na jopo la majaji katika shindano hilo lililoshirikisha warembo 106 kutoka kila kona duniani.

Miss World 2007

 

BAADA ya kuendesha shindano la urembo la dunia kwa mwaka wa nne, China hatimaye imemtoa mrembo katika shindano lililofanyika jana katika Ukumbi wa Hainan Province, China. Mrembo huyo, mwenye umbile la ulimwende wa kweli, Zi Lin Zhang alitangazwa jana na jopo la majaji katika shindano hilo lililoshirikisha warembo 106 kutoka kila kona duniani.

 

Shindano hilo lilikuwa likifuatiliwa na watu wasiopungua bilioni mbili, akiwamo Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefurahishwa na kaulimbiu ya kupiga vita ukimwi.

 

Mandela alikuwa akishuhudia mjukuu wake, Mandla Mandela, akitoa salamu za kupiga vita maambukizi mapya ya ukimwi wakati babu huyo akifurahia moja kwa moja kutoka Afrika Kusini.

 

Kabla ya shindano hilo la jana, warembo hao walikuwa kambini kwa takribani mwezi mmoja ambao si rahisi kwa kila mmoja kusahau ingawa mshindi alitakuwa kuwa mmoja tu aliyetangazwa na mwenyekiti wa Miss World, Julia Morley.

 

Mwanadada huyo aliangusha furaha kubwa mara baada ya mrembo wa mwaka jana, Tatana Kucharova kumvisha taji hilo huku nafasi ya pili ilikwenda kwa Micaela Reis wa Angola na kufuatiwa na Carolina Moran Gordillo wa Mexico.

 

Washiriki wengine waliongia fainali na kumtupa mbali mshiriki wa Tanzania, Richa Maria Adhia ni warembo kutoka Trinidad & Tobago, Valene Maharaj na Annie Oliv wa Sweden.

 

Shindano hilo la 57 tangu kuanza kufanyika kila mwaka, lilitangazwa na mtangazaji nyota wa China, Angela Chow aliyesaidiana na Fernando Allende, ambaye ni mmoja wa nyota wa Marekani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents