Burudani

Mchizi Mox: Muziki ni sehemu ya maisha yangu sijali usiponiingizia fedha

Rapper mkongwe wa kundi la Wateule, Mchizi Mox amesema hashangai na wala hababaiki kuona kuwa mpaka sasa hivi muziki haumlipi.

Mox

Akizungumza na Bongo5, Mox amedai kuwa toka anaanza kufanya muziki alikuwa anafanya ili kuwaburudisha mashabiki wake na sio kwaajili ya kupata fedha.

“Muziki ni sehemu ya maisha yangu, mimi nimenza muziki nilikuwa naupenda ulikuwa sio hata deal, ulikuwa haulipi wala nini,” amesema Mox. “Bora sasa hivi hata unalipa lakini sio kitu hata kinachonitia stress kwa sababu hata wakati mimi naanza sikuwa nategemea nitapata pesa kwenye muziki, hatukuwa tunapata hela. Mpaka tumekuja kuwa tunapata hela kwahiyo ni vile unavyojipanga ndo maana mimi ninaweza kukausha hata mwaka bila kutoa ngoma ,” ameongeza rapper huyo mwenye sauti nzito.”

“Hawa wanaolalamika hawapewi nafasi wanatakiwa wajipange. Mtu aliyezaliwa kutoa burudani au kuburudisha inabidi aburudishe, muziki ni burudani.”

Mox amewata mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya wimbo wake mpya na video ambao amedai utakuwa tofauti na kazi zake alizowahi kufanya.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents