Fahamu

MCHONGO: Atakayefanikiwa kudukua ‘Hacking’ simu za iPhone’s kulipwa Tsh. Bilioni 2

Kama wewe ni mtalamu wa uhalifu mitandaoni, Basi huenda ukawa bilionea endapo utafanikiwa kudukua simu pendwa duniani za iPhone na kompyuta za Mac.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Apple, wametangaza kuwa watatoa zawadi ya Dola milioni $1 sawa na Tsh Bilioni 2.3 kwa mtu yeyote atakayeweza kudukua simu za iPhone au kompyuta za Mac.

Mwanzoni kampuni hiyo, Ilitangaza kutoa kiasi cha Tsh milioni 460 kwa mtu yeyote atakayefanikiwa kudukua vifaa vyao.

Akieleza sababu za kuongeza zawadi kwa mtu atakayefakiwa kudukua simu hizo, Mkuu wa kitengo cha usalama wa Apple, Ivan Krstić, Amesema kuwa ongezeko hilo linatokana na uhakika wa ubora wa simu zao.

Kwa upande mwingine,  Ivan Krstić  amedai kuwa wanakusudia pia kuongeza zaidi zawadi hiyo, Kwani wanaamini wadukuzi wanalipwa pesa nyingi zaidi ya hizo pale wanapoenda kuuza teknolojia hizo serikalini.

Ivan Krstić ametangaza zawadi hiyo jana Alhamisi kwenye mkutano wa Black Hat uliofanyika mjini Las Vegas na kuelezea ulinzi wa mfumo wa iOS na MacOS.

Chanzo: https://www.forbes.com/sites/thomasbrewster/2019/08/05/apple-is-giving-out-hacker-friendly-iphones-plots-mac-bug-bounty-sources/#40093daf4f09

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents