Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mchungaji ajiua

Mchungaji wa Kanisa la Moravian la mjini Urambo mkoani hapa, Bw. Andrew Kilimba, amejiua kwa kunywa sumu baada ya mke wake kumbaini kuwa ana mwanamke mwingine nje ya ndoa na amemjegea nyumba.

Na Lucas Raphael, PST Tabora

 
Mchungaji wa Kanisa la Moravian la mjini Urambo mkoani hapa, Bw. Andrew Kilimba, amejiua kwa kunywa sumu baada ya mke wake kumbaini kuwa ana mwanamke mwingine nje ya ndoa na amemjegea nyumba.

 

Habari za kifo hicho zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Bw. Muhud Mshihiri, zilisema baada ya mkewe huyo kubaini hilo na kutaka kufahamu juu ya mwanamke huyo, mume wake alichukua uamuzi huo wa kujiua kwa kunywa sumu.

 

Alisema marehemu Kilimba alikuwa akiishi eneo la Majengo ya Tabora mjini Urambo, na pia ni mzee wa kanisa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Manchester ilioko wilayani humo.

 

Alisema inadaiwa kwamba marehemu Kilimba alikuwa amemjengea nyumba mwanamke mwingine (jina linahifadhiwa) mkazi wa maeneo ya Block Q mjini Urambo.

 

“Huyo bwana sisi tunadhani aliamua kujiua baada ya mkewe kuwa anambana mara kwa mara kuhusu fedha zinakokwenda zinazotokana na biashara yao ya nyumba ya kulala wageni na duka la dawa.

 

“Nakumbuka siku za nyuma niliwahi kuamua ugomvi kati yao kuhusu suala hilo la mapenzi. Mkewe alikuwa akihoji fedha zinazotokana na nyumba ya kulala wageni zinakwenda wapi?“

 

Alisimulia mmoja wa watu wa karibu na marehemu Kilimba.
Juhudi za kumsaka mke wa marehemu ili aweze kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kwamba yupo safarini Ukerewe mkoani Mwanza.

 

Baadhi ya watu na hasa waumini wa kanisa la Moravian waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu tukio hilo walisema marehemu Kilimba alikuwa mtumishi mzuri katika kanisa lao na kwamba pengo lake haliwezi kuzibika mara moja.

 

Hata hivyo, Kamanda Mshihiri alisema licha ya mtu huyo kujiua, polisi inaendelea na uchunguzi ili kupata taarifa zaidi za tukio hilo.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW