Habari

Mchungaji aliyefunga kula siku 30 afariki dunia, Ndugu zake wasema ataiona pepo

Mchungaji mmoja nchini Zambia aitwae,  Brighton Samajomba, wa kanisa na ‘HEAVEN IS MY HOME’ amefariki dunia baada ya kufunga kula kwa siku 30.

Mchungaji huyo mwenye imani kali, Amefarki dunia siku ya 20 baada ya kupatwa na Utapiamlo akiwa kwenye mfungo huo wa siku 30.

Akihojiwa na mtandao wa Zambia Watchdog, Kaka wa Marehemu, Reagan Samajomba amesema ndugu yake alikuwa na kawaida ya kufunga na kufanya maombi mara kwa mara.

Kuhusu kifo chake, Kaka wa Marehemu ameeleza kuwa ndugu yake aliamua kufunga siku 30 kwa lengo la kuiombea familia yake pamoja na waumini wa kanisa lake.

“Alifariki Jana (Jumatano Septemba 4) akiwa amefikisha siku 20, Kifo chake ni funzo kwetu kama familia tunaamini amekufa kwaajili yetu na kwa imani yake atafika peponi,” amesema Kaka wa Marehemu.

Polisi mjini Solwezi wamethibisha kutokea kwa tukio hilo, Na kuwaonya wananchi kuwa wawe makini na imani zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents