AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Mchungaji aliyepigwa risasi 40 na majambazi bila kupenya mwilini, akamatwa na polisi (+picha)

Wakati ulimwengu ukibuni njia ya kuweza kubuni mavazi ambayo yatazuia risasi kutokupenya kiurahisi kwenye mwili wa binadamu, hii ni tofauti kwa Mchungaji wa Kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry International, David Elijah kutoka Nigeria ambaye wiki iliyopita amenusurika kifo kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani.

Mchungaji David Elijah

Mchungaji David siku ya Ijumaa Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria alikuwa anaenda kanisani kwake akiwa kwenye gari alivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi.

Gari hilo lilitobolewa karibia lote kwa risasi lakini mpaka maaskari wanafika eneo la tukio, walimkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo.

Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo.

Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji huyo siku ya Jumamosi baada ya kujiridhisha kuwa mtu huyo alikuwa salama na ni raia mwema.

David akiwa kwenye gari baada ya kushambuliwa

Mchungaji David anatajwa kuwa moja ya wachungaji vijana wenye utajiri Mkubwa nchini Nigeria. Baada ya tukio hilo la kushambuliwa jana David alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika maburungutu ya fedha huku akiweka Captions kuwa yupo nchini Malaysia kikazi.

David akiwa chini ya ulinzi

Maoni mengi ya wadau mitandaoni nchini Nigeria yanaonekana kushangazwa na tukio hilo, huku wengi wao wakidai kuwa Mchungaji huyo anatumia nguvu za giza.

Chanzo-http://www.gistmania.com/talk/topic,366322.0.html?utm_source=dlvr.it&utm_medium=twitter

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW