Mchungaji Isaac kutoka Ghana alitabiri Trump atashinda urais, akataa kuitwa muongo (+Video)

Nabii huyo wa Ghana, Isaac Owusu Bempah amekanusha madai kuwa amesema atawalaani watu wanaomkosoa kuwa yeye ni ‘mchungaji bandia’ baada ya kutabiri ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa mwaka huu na mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Wakosoaji walisambaza video zikimuonesha nabii huyo akisema Donald Trump atashinda uchaguzi.

Hata hivyo mchungaji huyo alishindwa katika utabiri wake lakini anadai kuwa hakusema kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican anaenda kushinda.

“Kama Mungu ndio anaongea na mimi katika fikra zangu… basi sijaiba au kumbaka yeyote.

Kama Mungu amenionesha jambo kulizungumza nafanya hivyo , Mungu anakuja kwako,” Isaac Owusu Bempah amesema.

“Kijana yule anayekanusha kunitusi mimi, atakufa kifo kibaya , ataangaika sana duniani ” aliongeza.

Mchungaji huyo maarufu nchini Ghana ambaye huwa anatabiri kile kinachoweza kutokea baadae, mfano mwaka 2019 alidai kuwa Imam mkuu wa Ghana atafariki.

Nabii huyu wa Ghana huwa anapenda kutabiri nani atakuwa mshindi katika uchaguzi, na mtu gani maarufu atafariki.

Mara nyigine utabri wake huwa unamuweka kwenye wakati mgumu nabii huyu, lakini kuna wakristo wanaomwamini .

https://www.instagram.com/tv/CHkHu7yh3vk/

https://www.instagram.com/tv/CHkHu7yh3vk/

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW