Habari

Mchungaji James Ng’ang’a awamwagia matusi maaskofu , awataka wamuheshimu mke wake, lasivyo atawatimua wote nchini Kenya

Mchungaji James Ng'ang'a awamwagia matusi maaskofu , awataka wamuheshimu mke wake, lasivyo atawatimua wote nchini Kenya

Mchungaji maarufu nchini Kenya Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelist Ministry amegonga vichwa vya habari kwa mara nyengine tena baada ya kutishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism akidai kwamba maaskofu hawamuheshimu mke wake. Katika kanda ya video iliosambaa katika vyombo vya habari , anaonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafurusha wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda.

”Wakati huu nitawaonyesha uwezo wangu… mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu ….mulinipata hapa na wake zenu, mumejitajirisha kupitia juhudi zangu” .

”Wajinga nyie…wajeuri…nilikuwa nikihubiri katika mkokoteni , naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ng’ang’a ni nani….”.

Kwa mujibu wa BBC. Mchungaji huyo anaonekana akiwaambia kwamba ni kinyume kwa wao kujigamba kuhusu utajiri waliojipatia kutoka katika kanisa lake na bado hawamuheshimu.

”Nataka kuwaambia nyinyi maaskofu, iwapo hamutamuheshimu mke wanngu nitawafurusha katika kanisa langu. sitaki kujua wewe ni nani”, alisema mchungaji huyo.

Ng’nga anasema kuwa amefikisha umri ambao anahitaji kuheshimika na maaskofu wote. Ninapo kohoa lazima mutii, alisema.

Mchungaji huyo alisema kuwa anakabiliwa na changamoto kwa sababu shetani anataka kuliangusha kanisa lake.

”Shetani anakabiliana nami kwa sababu anataka kuniangusha, hakuna kitu munachoweza kuniambia….Mimi ni Neno na ndio maana ninapigwa…. Sitawaruhusu nyinyi na wake zenu kunipatia msongo wa mawazo zaidi”,alisema.

”Iwapo munataka kujiita maaskofu, munahitaji kufikiria kule mulikotoka, ni vipi munajigamba mbele yangu na mulikuja kwangu na umaskini…nitawafukuza nyie nyote… takataka”, aliendelea.

Amesema kuwa atayafunga matawi yote na kusalia na makao makuu pekee.

Ng’ang’a aliwataja maaskofu wake kuwa watu wasio na maana, wajinga na wasiomuheshimu kama mtu aliyewasaidia.

”Ni lazima waniheshimu la sivyo nitaelekea kuvifunga mimi mwenyewe vibanda vyote nibakie na kanisa kubwa lililopo jijini Nairobi. Mimi ndio mwanzilishi wa Neno”, alisema huku akipongezwa na wafuasi wake.

Ng’ang’a amesema kuwa maaskofu katika matawi ya kanisa lake hawana heshima lakini akawataka kujua kwamba yeye ndio kamanda mkuu.

Mchungaji huyo amegonga vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni kwa sababu ambazo sio nzuri.

Kiongozi huyo wa dini mwezi uliopita alikamatwa na maafisa wa polisi na kushtakiwa mahakamani kwa madai ya kumuibia mfanyabishara mmoja kwa njia ya udanganyifu $36,000.

”Alikuwa amekubali kulipa lakini akachelewa kuheshimu makubaliano hayo. Hivyobasi tuliamua kumchukulia hatua mahakamani”, alisema kamanda wa kituo cha polisi cha Central Stanley Atavachi.

Katika kesi nyengine , alishtakiwa kwa kutishia kumuua mwandishi wa runinga ya Citizen nchini Kenya Linus Kaikai.

Pia anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na ukiukaji wa sheria.

Hakimu wa mahakama hiyo aliwamchilia kwa dhamana ya $2000

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents