Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mchungaji Rwakatare “Tuliomba Kimbunga kutoka msumbiji kikapiga chenga, Nzige wameganda hawajafika kwetu itakuwa Corona” – Video

Mchungaji Rwakatare "Tuliomba Kimbunga kutoka msumbiji kikapiga chenga, Nzige wameganda hawajafika kwetu itakuwa Corona" - Video

Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Dkt Getrude Rwakatare amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwaasa Watanzania wachape kazi na wasiogope sana kuhusu Virusi vya Corona wakati Mungu yupo.

Rwakatare meongeza kuwa “Mimi nakumbuka kipindi kile kuna kimbunga kinatoka Msumbiji na kilisemekana lazima kingepiga Tanzania lakini tuliomba na tuylipoomba kile kimbunga kilipiga chenga kikaondoka kikaenda nchi nyingine lazima tumshukuru Mungu.

“Sio hivo Nzige hapa juzi wapo Kenya lakini wameganda mbona hawaji huku ni kwa sababu tumeomba na Nzige waishie huko huko sasa je atashindwa Corona? Rais wetu alinifurahisha aliposema kuwa jamani Corona sio kubwa kuliko Mungu”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW