Burudani

MDB yamsainisha staa wa rap ya Kisukuma, Nkunda Star

Label ya Millian Dollar Boys, MDB iliyokuwa maskani kwa Young Dee, imemsainisha staa wa rap/trap ya Kisukuma, Nkunda Star kutoka Shinyanga.

Nkunda Star alijipatia umaarufu kwa wimbo wake Dimaga aliorap kwa Kisukuma kiasi cha kumvutia CEO wa MDB, Max Rioba ambaye alimuita Dar na kuurudia wimbo Dimaga pamoja na kufanya video yake itakayotoka Ijumaa hii.

“Kuna nyimbo unapozisikia kwa Mara ya kwanza tu unatamani uwe sehemu ya maandalizi yake. @nkunda_star ni msanii kutoka Mwanza ambaye alinishangaza sana kwa uwezo wake wa kutumia kabila la kisukuma kutunga wimbo katika midundo ya hip hop trap,” ameandika Max kwenye Instagram.

“Nilipousikia Wimbo wake uitwao Dimaga kwa Mara ya kwanza nilimwambia asafiri kuja Dar niufanyie remake mpya. Nkunda ni msanii chipukizi lakini mwenye uwezo wa Hali ya juu sana. Niliongea na team yangu tukaufanya wimbo huu upya, nikatoa pia camera tukashoot video ambayo quality yake ni nooma sana. Kesho Ijumaa mtapata fursa ya kuiona video hiyo ambayo imeshutiwa na cinematographer ambaye wengi wanamchukulia poa lakini ni mmoja Kati ya Cinematographers wanaojua vizuri kutumia Red camera hata katika mazingira magumu. Si mwingine huyu Bali ni @director_minzimims big up sana kwa mkono wa pekee,” ameongeza.

“Shukran nyingi sana pia kwake sound engineer and producer Allan Mapigo @mapigoallan kwa kuipiga beat hii kitaalamu sana. Wimbo huu DIMAGA utapatikana kesho tarehe 7, April kila mahali. #2017bongemojalamwaka ???????????????? #MDBwillNeverDie.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents