Michezo

Mdhamini ligi kuu bado kizungumkuti, rais Karia anena haya ‘Bodi imechemka’

Mdhamini ligi kuu bado kizungumkuti, rais Karia anena haya 'Bodi imechemka'

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Wallace Karia amesema kuwa Bodi ya ligi (TPLB) ndiyo imesababisha kuchelewa kwa mkataba na wadhamini wa kuu Vodacom mpaka sasa.

Karia ameyasema hayo wakati alipohojiwa na radio E FM kupitia kipindi chao cha michezo.

”Siyo kweli kwamba TFF ndiyo inayoongea na wadhamini, wakati mimi nilivyokuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ligi ndiyo nilikuwa naongea na wadhamini, mimi, Mzee Saidi, Mwakibinga na viongozi wengine wakina Kaburu ndiyo tulikuwa mstari wambele kuhangaikia hilo,” amesema rais Karia.

TFF yatangaza ratiba ya ligi

Rais Wallace Karia ameongeza ”Bodi imechemka, viongozi wake waliyokuwepo kwenye Bodi hawakufanya majukumu yao ilivyotakiwa ndiyomaana imechelwa. Sasahivi tunashirikiana na mtu anayekaimu uongozi wa Bodi tunamsaidia kwa kushirikiana Sekretarieti ya TFF na baadhi ya wajumbe wa kamati ya TFF wanawasaidia kuhakikisha hayo mazungumzo yanafanyika haraka.”

”Kiongozi ambaye amechemka tayari tumeshamuondoa alikuwa Mwenyekiti, lakini sisi tunajitahidi kuongea na Vodacom na matumaini yapo watu wasubiri.”

Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya ligi kuu (TPLB), Clement Sanga alienguliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini baada ya klabu ya Yanga kupeleka barua ya kumkataa.

Kwa mujibu wa Shirikisho hilo lenyedhamana ya kusimamia soka la Tanzania ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 inatarajia kuanza Agosti 22 2018.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents