BurudaniHabari

Mdogo wa Jordan Sparks afariki dunia

Mwanamuziki Jordin Sparks afiwa na mdogo wake wa kambo mwenye umri wa miaka 16 Bryanna Jackson-Frias.
Marehemu Bryanna Jackson amefariki siku ya Jumanne jioni kwa ugonjwa ambao alikuwa akipambana na nayo maisha yake yote uitwayo Sickle cell anemia.

Sickle cell Anemia ni ugonjwa wa kurithi wa kupungukiwa damu, ambapo mgonjwa hua hana damu ya kutosha kwa sababu ya seli zake za mwili sio imara kubeba hewa ya oksijeni kupeleka sehemu mbalimbali za mwili. ukosefu wa oksijeni unaweza kuharibu viungo na kusababisha maumivu makubwa sana ambayo husabibisha binadamu kulazwa hospitali.

Mama wa Jordin Sparks, Jodi Jackson alitumia akaunti yake ya Facebook kutoa ujumbe huo siku ya Jumatano ambapo alituma picha ya binti yake.

https://www.facebook.com/photo.php?fbid=10215491629063221&set=a.2326501921343.2140008.1213512764&type=3&theater

kabla ya kifo cha dada yake, Jordin Sparks ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza na mumewe Dana Isa, Jumanne alituma picha hii hapa chini.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents