Michezo

Mechi mbili za Sierra Leone dhidi ya Ghana zafutiliwa mbali na Shirikisho la soka duniani FIFA

Mechi mbili za Sierra Leone dhidi ya Ghana zafutiliwa mbali na Shirikisho la soka duniani FIFA

Shirikisho la kabumbu barani Afrika limeahirisha mechi kati ya Sierra Leone na Ghana kufuatia uamuzi uliopitishwa na FIFA.

Mechi mbili za timu ya taifa ya Sierra Leone dhidi ya Ghana katika kinyang’anyiro cha kuwania kombe la mataifa barani Afrika zimefutwa na haijulikani bado kama zitafanyika.

Shirikisho la kabumbu barani Afrika limeahirisha pambano kati ya Sierra Leone na Ghana lililokuwa lifanyike siku ya Alkhamisi na Jumatatu inayokuja kufuatia uamuzi uliopitishwa wiki iliyopita na shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA wa kulizuwia shirikisho la kabumbu la Sierra Leone kwa sababu ya ushawishi wa kisiasa.

Shirikisho la kabumbu barani Afriksa CAF halikusema kama Sierra Leone itaruhusiwa kucheza baadae au kama Ghana itatajwa mshindi wa mechi zote mbili.

Uamuzi huo utaziathiri timu zote nne za kundi F ambalo ponti moja tu ndiyo inayozitenganisha Kenya, Ethiopia, Ghana na Sierra Leone katika kinyang’anyiro cha kushiriki katika fainali ya kombe hilo mwakani.

Chanzo DW Swahili

By All Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents