Michezo

Mechi ya Azam FC vs Simba yabadilishwa muda

Mchezo namba 10 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ‘VPL’ kati ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC dhidi ya Simba SC, sasa utafanyika majira ya saa 10.00 jioni badala ya muda wa awali uliopangwa wa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo yenyemaskani yake Chamazi Jijini Dar es salaam umesema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ limebadilisha muda huo kutokana na kuagizwa na Jeshi la Polisi kuipeleka mechi hiyo jioni kutokana na sababu za kiusalama, ikidai ni hatari kufanyika usiku.

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kumalizia maandalizi ya mwisho leo Ijumaa jioni kuelekea mchezo huo, ambao utachezeshwa na mwamuzi Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani.

Mwamuzi wa mezani atakuwa,Josephat Bulali huku Kamisaa atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents