Michezo

Mechi ya England Vs Bulgaria yapelekea watu wanne kutiwa mbaroni, wengine wasakwa popote walipo na Polisi

Jeshi la polisi nchini Bulgarian limewakamata watu wanne kwakuwa na mahusiano ya moja kwa moja na mashabiki ambao walikuwa wakitoa kauli za kibaguzi zilizojaa matusi kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya 2020 baina ya England dhidi ya wenyeji wao Bulgaria uliyopigwa kwenye uwanja wa Sofia.

Monday's match was halted twice after abuse was aimed at the England squad

Kwenye mchezo huo England ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya bao 6 – 0 dhidi ya wenyeji wao Bulgaria licha ya kuwa mechi hiyo ilisimamishwa mara mbili katika kipindi cha kwanza kufuatia kauli hizo za kibaguzi zilizokuwa zikitolewa na mashabiki wa timu mwenyeji.

Image result for Bulgarian police arrest four people in connection with racist abuse of England players

‘European football governing body UEFA’ imeanza taratibu za kuipatia adhabu Bulgaria kufuatia tukio hilo, wakati Rais Aleksander Ceferin akionyesha kutovumilia vitendo vya kibaguzi katika soka.

Na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bulgaria imesema Jumatano hii kwamba tayari imewakamata watu wanne na msako mkali unaendelea kwa wengine wote wliohusika.

Maneno ya kibaguzi yalikuwa yakisikika hadharani uwanjani kipindi cha kwanza wakati beki wa England, Tyrone Mings akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliyokuathirika zaidi na maneno hayo hadi kupelekea kumweleza mwamuzi  kutoka Croatia, Ivan Bebek.

Image result for Bulgarian police arrest four people in connection with racist abuse of England players

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents