Michezo

Mechi ya kwanza ya NBA kuwahi kuchezwa Afrika kufanyika Aug. 1 Johannesburg

Mechi ya kwanza ya NBA itachezwa barani Afrika kwa mara ya kwanza August 1 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

giannis-africa-1200x600

Mechi hiyo itawakutanisha wachezaji wa NBA waliozaliwa Afrika, Team Africa dhidi ya wengine wa Team World. Mchezaji anayechezea Miami Heat, Luol Deng aliyezaliwa Sudan ataiongoza Team Africa.

“Ninajivunia sana kuwa sehemu ya mechi ya kwanza ya NBA barani Afrika,” alisema.

Team Africa inaundwa pia na:

Al-Farouq Aminu (Nigeria) wa Portland Trail Blazers, Giannis “The Greek Freak” Antetokounmpo (Nigeria) wa Milwaukee Bucks na Nicolas Batum (Cameroon) wa Charlotte Hornets.

Wengine ni Bismack Biyombo (Congo) wa Toronto Raptors, Boris Diaw (Senegal) wa San Antonio Spurs, Gorgui Dieng (Senegal) wa Minnesota Timberwolves, Festus Ezeli (Nigeria) wa Golden State Warriors, Luc Mbah a Moute (Cameroon) wa Sacramento Kings na Serge Ibaka (Congo Brazzaville) wa Oklahoma City Thunder.

Team Africa itanolewa na kocha wa San Antonio Spurs, Gregg Popovich.

Team World inaongozwa na Chris Paul anayechezea Los Angeles Clippers na wachezaji wenzake ni pamoja na:

Washington Wizards guard Bradley Beal
Denver Nuggets forward Kenneth Faried
Memphis Grizzlies center Marc Gasol
Chicago Bulls center Pau Gasol
Memphis Grizzlies forward Jeff Green
Boston Celtics guard Marcus Smart
Boston Celtics forward Evan Turner
Orlando Magic center Nikola Vucevic

Timu hiyo inanolewa na kocha Brooklyn Nets, Lionel Hollins.

Mchezo huo utarushwa live kwenye SuperSport.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents