Michezo

Mechi ya Simba na Yanga kukusanya tsh 545,422,000

Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limetangaza mahudhurio na mapato yaliyopatikana katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba, Jumapili Machi 8, 2020.

Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa taifa na kumalizika kwa Simba kukubali kichapo cha bao moja, ikiwa ni kichapo cha kwanza kutoka kwa mahasimu wao katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Jumla ya watazamaji elfu hamsini na tisa na mia tatu ishirini na tano (59325) walihudhuria mchezo huo na kuingiza jumla ya Shilingi milioni mia tano na laki nne na ishirini na mbili elfu (545,422,000).

Kwa mujibu wa sheria mpya za mapato ya uwanjani za Bodi ya Ligi, baada ya kodi na makato ya uwanja, mapato yote yanayobakia yanakwenda kwa timu mwenyeji wa mchezo huo ambao ni Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents