Burudani

Meek Mill amkana Rick Ross; Adai bifu yake na Drake bado ipo pale pale

Imepita siku moja tu baada ya Rapa Rick Ross kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, Bifu yake na Drake imeisha na kuweka wazi pia hata Meek Mill nae amemalizana Drake. kambi ya Meek inasema tuahau hilo, bifu la Drake na Meek Mill bado lipo pale pale.

Image result for Drake and meek mill
Meek Mill na Drake kabla ya bifu yao.

Mtandao wa TMZ umeeleza kuwa watu wa karibu wa rapa Meek Mill wamesema rapa huyo amekataa kuwa hawajakutana na Drake wala Uongozi wake na hajawahi kufikiria kupatana na Drake.

Inadaiwa kuwa, mashairi ya wimbo wa Drake wa ‘Back To Back’ ambao alidisiwa bado unamuumiza kichwa na hawezi kumuelewa Rick Ross anavyosema kuwa aliwapatanisha wawili hao.

Hata hivyo waandishi wengi wa habari za burudani ulimwenguni wanasema Meek Mill hawezi kumaliza bifu lake na Drake kirahisi kwani ukaribu uliopo kati Drake na ex wake Nicki Minaj bado unamuathiri kisaikolojia kila kukicha.

Bifu ya Drake ilianza mapema mwaka 2015 baada ya kuingia kwenye uhusiano na rapa, Nicki Minaj na kuanza kutupiana maneno ya hapa na pale mitandaoni kabla ya kutungiana ‘Diss Track’ zilizokoleza bifu hilo.

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents