Tupo Nawe

Meja Kunta: Naupenda wimbo wa Singeli wa Harmonize, ameipeleka singeli Kimataifa (Video)

Msanii wa Singeli Meja Kunta amedai ni kweli Harmonize ameipeleka singeli kimataifa kupitia wimbo wake, Hujanikomoa ambao kwa sasa unafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga.

Muimbaji huyo amewataka baadhi ya watu mitandaoni kuacha kumshindanidha na Harmonize kupitia wimbo wao walioshirikiana na Lavalava uitwao, Wanga.

Meja amedai bosi huyo wa Konde Gang ni level za akina Diamond na anatambua mchango wake katika muziki wa singeli kupitia wimbo, Haujanikomoa.

Wiki iliyopita baadhi ya mashabiki mitandaoni walikuwa wanazishindanisha ngoma hizo mbili.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW