Burudani

Melanin World Tour ya bendi la Sauti Sol inakuja Dar es Salaam Disemba hii

Bendi maarufu kutoka Kenya, Sauti Sol, inawaletea onyesho la kipekee tarehe 15 Disemba 2018 pale Buckets, Masaki.

Kabla ya kufika Dar es Salaam, Melanin Tour imewapa Sauti Sol fursa ya kucheza mziki wao kimataifa – kutoka Melbourne, Australia hadi Paris, Ufaransa. Na sasa, Dar es Salaam!

Sauti Sol inawaletea mziki wa kiroho, kutumia sauti zao na vyombo vya muziki (LIVE), ili kuwapa mashabiki tamasha pekee la mwaka.

MIAKA KUMI YA SAUTI SOL

Mwaka huu ulikuwa mwaka muhimu wa Sauti Sol. Walitoa midundo yao “Short N’ Sweet” na “Tujiangalie”, na nyimbo yao “Melanin” ulipata mafanikio ya kimataifa barani Afrika. Wamecheza kwenye matamasha mbali mbali pamoja na wasanii wakubwa kama Major Lazor.

Mwaka huu pia waliadhimisha miaka 10 tangu kutolewa albamu yao ya kwanza, “Mwanzo”. Tangu enzi za nyimbo za “Lazizi”, “Mama Papa” na “Blue Uniform”, waTanzania wameendelea kuwa washabiki wakuu wa Sauti Sol. Bendi hili liko tayari kuonyesha tena Dar es Salaam na kurudisha upendo waliopata kutoka washabiki wa Tanzania.

Nyimbo zao, zinazounganisha maneno ya kiroho, sauti zao nzuri na gitaa, zimewaletea mafanikio makubwa ambayo hawakuweza hata kuotea. Bien, Chimano, Polycarp na Savara wamecheza na marais, wameshiriki kwenye matamasha mengi kwenye bara la Afrika na nje, wameshinda tuzo nyingi za kusherekea vipaji vyao na wameshirikiana na baadhi ya wasaani wakubwa kama Alikiba.

Wao ni wasanii wa kweli wa kiAfrika na wanaweka asili hii kwenye maonyesho yao yote ya kimataifa. Karibuni, wameungana na wasanii kutoka nchi za Afrika – Tiwa Savage, Burna Boy, Nyashinski kuwaletea mradi unaoitwa “Afrikan Sauce”, ambao unawaletea midundo mipya ya kipekee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents