Habari

Meli kubwa ya kitalii iliyokosa pa kwenda hatimaye yatia nanga, baada ya kukataliwa katika bandari 5 

Meli moja ya kitalii ambayo ilikuwa imekwama isijue pa kwenda baharini, kutokana na wasiwasi wa bandari kuhusu uwezekano wa kubeba abiria walioambukizwa virusi vya corona hatimaye imetia nanga nchini Cambodia.

Meli ya Kitalii ya Westerdam

Meli hiyo kwa jina MS Westerdam ilizuiwa kutia nanga katika bandari tano barani Asia. Meli nyengine ya kitalii iliotengwa nchini Japan ina zaidi ya maambukizi 200.

Lakini Westerdam ilio na zaidi ya abiria 2000 pamoja na wafanyakazi haina maambukizi yoyote. Siku ya Jumanne , meli hiyo ilijaribu kutia nanga nchini Bangkok lakini ikanyimwa ruhusa.

Image result for MS Westerdam ship

Meli ya wanamaji wa Thai iliisindikiza hadi nje ya ghuba la Thailand ambapo ni kutoka hapo ilipoamua kuelekea Cambodia. Siku ya Alhamisi , meli hiyo hatimaye iliwasili katika eneo la kutia nanga katika mji wa bandari ya Sihanoukville.

”Mapema leo asubuhi , kuona ardhi ilikuwa kitu muhimu sana” , alisema abiria Angela Jones kutoka Marekani akizungumza na Reuters, ”Nilidhani Je huu ni ukweli?.”

The Westerdam, inayoendeshwa na kampuni ya America Line kutoka Uholanzi , iliondoka mjini Hong Kong tarehe mosi Februari ikiwa na abiria 1455 na wafanyakazi 802.

Meli hiyo ilikuwa imetarajiwa kuzunguka kwa wiki mbili na katika siku hizo 14 kulikuwa na matatizo ya kuisha kwa mafuta mbali na chakula.

Mbali na Thailand , pia ilifukuzwa na Taiwan, Guam na Japan.

”Tumekuwa na bahati mbaya chungu nzima, tulidhani tunaenda nyumbani kabla ya kufukuzwa”, alisema bi Jones .

Nahodha wa meli hiyo Vincent Smit alisema kwamba meli hiyo itatia nanga nje

Sihanoukville iliruhusu mamlaka kufanya ukaguzi wa kiafya ndani ya meli hiyo.Abiria wakijiburudisha kwa michezoAbiria waliamua kutafuta kitu cha kufanya ili kukabiliana na muda

Abiria badaye wataweza kuondoka katika meli hiyo na kurudi nchini mwao kutoka mji mkuu wa taifa hilo Phnom Penh. Ubalozi wa Marekani nchini Cambodia ulisema kwamba umetuma kikosi kitakachosaidia raia wake kupanga safari zao.

Uamuzi huo wa Cambodia kuwaruhusu abiria hao kutia nanga nchini humo ulipongezwa na mkuu wa shirika la afya duniani WHO.

” Ulikuwa mfano wa umoja wa kimataifa ambao tumekuwa tukiitisha” , alisema mkurugenzi mkuu wa WHO Jenerali Tedros Ghebreyesus.

Kumekuwa na ukaguzi wa kiafya wa mara kwa mara kwa abiria wote na hakujaonekana hata kisa kimoja.

Meli iliopo Japan iliotengwa katika bandari ya Yokohama , kufikia sasa ina visa 200 vilivyothibitishwa , na kuifanya meli hiyo ya Diamond Princess kuwa kubwa kwa maambukizi mengi zaidi nje ya China .

Sio abiria wote waliofanyiwa vipimo na idadi ya visa huenda ikaongezeka. Visa vingine 44 viliongezwa katika jumla hiyo siku ya Alhamisi.

Meli nyengine ya utalii ilitengwa kwa siku kadhaa karibu na pwani ya Hong Kong , kwa kuwa mgeni mmoja alikuwa amepatikana na virusi vya corona. Abiria wote sasa wameruhusiwa kutoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents