Habari

Meli kubwa ya Marekani yaanza safari zake nchini Cuba

Meli kubwa ya kifahari kutoka Marekani, Adonia imeaanza safari zake rasmi kati ya nchi ya Marekani na Cuba.

11728265w_r900x493

Cuba na Marekani zimekuwa kwenye uhasama wa vita baridi kwa kipindi cha miaka 54. Kipindi chote hiko kulikuwa hakuna usafiri wa majini wa moja kwa moja kutoka Marekani mpaka Cuba.

Nchi hizo zimerejesha uhusiano wa wa kidiplomasia mwaka jana ambapo mwezi March mwaka huu rais wa Marekani, Barack Obama alifanya ziara yake ya kwanza nchini Cuba huku watu mbalimbali wakionekana kufurahia hatua hiyo.

Pia imeripotiwa kuwa meli hiyo itafanya safari zake kutoka Miami hadi nchi ya Cuba kila baada ya wiki mbili na tiketi zake zitauzwa kwa kiasi cha dola 1,800.

Meli hiyo iliyong’oa nanga kwenye bandari ya Miami ikiwa na abiria zaidi ya 700 inatarajiwa kufika nchini Cuba wiki ijayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents