Habari

Meli ya LCT Spice Island yazama Nungwi

meli_imezama

Tanzania imeingia kwenye msiba mzito baada ya meli LCT Spice Island  ambayo ilikuwa ikifanya safari zake za Dar es salaam, Unguja na Pemba, kuzama katika mkondo wa maji wa Nungwi uliopo kati ya Pemba na Unguja.


Watu zaidi ya 610, wamezama maji katika ajali hiyo, iliyotokea mnamo saa 08: 30 usiku mpaka saa 9 usiku, huku boat za uokoaji zikiwahi kuja kujaribu kuokoa baadhi ya watu waliokuwepo kwenye meli hiyo.

Inasemekana meli hiyo iliondoka katika bandali ya Malindi salama, lakini matatizo yakaja kutokea njiani wakati ilipofika ukanda bahari katika mkondo wa bahari unaojulikana kama  Nungwi, na kusababisha kupinduka kwa meli hiyo.

Hadi sasa abilia wapatao 250, ndiyo waliookolewa huku raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein yupo hapo kwenye tukio akifuatilia matukio yote yanavyokwenda juu ya kupatikana kwa mili iliyosalia.

Hadi sasa idadi kamili ya watu ambao wamekufa maji bado hajajulikana, hivyo waliofanikiwa kuokolewa wanatarajiwa kukutana na familia zao kwenye viwanja vya Maisara  kwaajili ya kuendelea kusubiri taarifa zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents