Michezo

Mendes, Iwe Jua Iwe Mvua hakikisha narudi United – Ronaldo

By  | 

Mchezaji bora wa dunia raia wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemtaka wakala wake mashuhuri, Jorge Mendes afanye kila lililo juu ya uwezo wake kuhakikisha anarejea Manchester United.

Cristiano Ronaldo  ana muhimiza Meneja wake ahakikishe anarejea Manchester United

Nyota huyo wa Real Madrid ameyasema hayo siku ya Ijumaa ikiwa ni mara baada ya kuingia katika shutuma za ukwepaji wa kodi inayofikia paundi milioni 13 hali iliyosababisha kumuambia wakala wake Mendes ahakikishe anafanya kila liwezekanalo ndoto za kurudi United zinatimia.

Cristiano Ronaldo aliondoka Manchester United na kutua Real Madrid mwaka 2009

Ronaldo aliondoka Old Trafford na kutua Real Madrid miaka nane iliyopita , aliwatikisa vigogo wa Hispania baada ya kutangaza kauli yake hiyo.

Cristiano Ronaldo akipiga picha na Meneja wake Jorge Mendes (kulia)

Mpaka sasa klabu ya United, Chelsea, Paris Saint-Germain pamoja na Bayern Munich zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mreno huyo ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya taifa katika michuano ya mabara inayoendelea huko nchini Urusi.

Man Utd, Chelsea, PSG pamoja na Bayern Munich zimeonesha nia ya kuhitaji huduma Ronaldo mwenye miaka  32

Matajiri wa Ufaransa PSG imetenga kitita cha paundi milioni 122m kwaajili ya uhamisho wake huku wakitarajia kumlipa mshahara wa paundi 26m kwa mwaka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anadhani bado kuna kazi hajaimaliza Old Trafford lakini pia haitaji kuikosa nafasi ya kurejea kama shujaa ndani ya klabu yake ya zamani ya United.

BY HAMZA FUMO

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments