Michezo

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho ashtakiwa na FA

Kocha wa Chelsea asiyeishiwa vituko, Jose Mourinho ameshtakiwa na chama cha soka cha England, FA kufuatia madai yake kuwa kuna ‘kampeni’ ya waamuzi dhidi ya timu yake.

244C5A9200000578-2902224-image-m-14_1420737255967

Mourinho alitoa matamshi hayo baada ya Chelsea kunyimwa penati dhidi ya Southampton Disemba 28 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Mwamuzi Anthony Taylor alimuonesha kadi ya manjano Cesc Fabegas baada ya kuanguka ndani ya boksi wakati akikabiliwa na Matt Targett.

Mourinho anatakiwa hadi Januari 13 kujibu mashtaka hayo.

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents