Burudani

Menejimenti ya rapa Falz yawajibu waislamu wanaotaka afute video ya wimbo wake wa ‘This is Nigeria’

Baada ya kikundi cha waislamu cha The Muslim Rights Concern (MURICO) cha nchini Nigeria kumtaka rapa Falz kufuta video ya wimbo wake mpya wa ‘This is Nigeria’, hatimaye uongozi wa rapa huyo umekijibu kikundi hicho.

Uongozi huo umesema kuwa hakuna sehemu yoyote katika sheria za Nigeria inayokataza mtu kucheza akiwa amevaa Hijab hivyo kikundi hicho labda kina lengo lingine juu ya msanii wao.

Hakuna chochote ambacho tunaweza kusema kwa sasa, zaidi ya kuwaeleza kuwa hatuwezi kufuta video hiyo kwa kile tunachoona kuwa hakuna tatizo.  Na kama kutakuwa na tatizo basi waende mahakamani nadhani huko tutaongea vizuri zaidi,“amesema Femi Soro moja ya viongozi wa Menejimenti ya FALZ.

Juzi waislamu nchini Nigeria walimpa siku 7 rapa Falz kufuta video ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube wakidai kuwa ameidhalilisha dini ya Kiislamu kwa kuwavalisha wanawake hijab na kuwachezesha kwenye video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents