Burudani

Menina awasimulia BASATA mkasa mzima wa video yake ya ngono iliyovuja (Picha)

Msanii Menina Abdulkarim ambaye anafanya kazi za sanaa kama Msanii wa Bongo flava, MC, na Muigizaji wa filamu hapa nchini hatimaye Jumatano hii amefika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) zilizopo Sharif Shamba,Ilala jijini Dar Es Salaam ili kutoa maelezo yake juu ya kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

Baraza hilo kupitia, Katibu Mtendaji-BASATA, Godfrey L.Mngereza limetoa taarifa hiyo hapo chini baada ya kikao kizito.

Mara kadhaa BASATA kupitia utaratibu wake wa kutoa Elimu kwa wasanii na Umma wamekuwa wakiwaelekeza wasanii wote kote nchini kufanya kazi zao za Sanaa kwa kuzingatika maadali mema kwa jamii,pamoja na kufuata taratibu za kujisajili,lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa hawazingatii maelekezo hayo na hivyo kujikuta wanavunja sheria za nchi.

Kupitia mahojiano kati ya Msanii na BASATA kwa pamoja wamesikiliza maelezo ya Msanii Menina Abdulkarim na nini kilichojitokeza katika sakata zima la kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa kuwa suala la kusambaa video na picha za utupu za Msanii Menina katika mitandao ya kijamii lipo mikononi mwa mamlaka nyingine,BASATA imeamua kuyafanyia kazi maelezo yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents