Soka saa 24!

Meseji za Chris na Offset wakigombana zavuja, Offset alimuita Chris ‘Teja’ na Chris kuuweka bayana mtaa anaoishi Offset, sababu ikiwa ni sakata la 21 Savage

Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Christopher Maurice Brown alimaarufu Chris Brown, mmoja ya wasanii wasioishiwa vitu ameingia kwenye ugomvi mzito na msanii mwenzake kutoka Marekani Rappre Kiari Kendrell Cephus alimaarufu OffSet.

Msala ulianza baada ya Chris Brown kuweka video ya utani kumuhusu rapper 21 Savage. Offset alionekana kutopendezwa na utani huo na kuamua kumjibu Chris Brown kwa kuandika: “Video za utani sio poa” aliandika Offset ambaye baadae alioga matusi mazito toka kwa Breezy.

Breezy alimaindi baada ya Offset alitupia neno la mwisho kwa kumuita Chris Brown ‘Teja’

Kila siku kukicha yanaibuka mengine na ikumbukwe Chris alitangaza atamtwanga ngumi rapper #Offset kupitia Instagram yake.

LeoBreezy amepost video ya kejeli kuhusu #Offset inamuonyesha mtu akiita Polisi mara baada ya #Chris kutaja mtaa ambao #Offset anaishi. kitu ambacho hakijaeleweka kwanini Chris amefanya hivyo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW