Burudani

 Mesen Selekta ameshindwa kubadilika – Manecky

By  | 

Prodyuza kutoka AM Records, Manecky amesema prodyuza mwenzake Mesen Selecta ni miongoni mwa maprodyuza ambao anawakubali kwa sasa ila ameshindwa kubadilika.

Manecky

Maneck alisema hayo wakati akichambua mwenendo wa maprodyuza wengi nchini kwa sasa, akisema wengi wameshindwa kujiongeza hatima yake wanakuwa wanarudia vitu ambavyo tayari vimekwishafanyika.

“Mimi mwenyewe huwa nasikiliza sana kuna vitu ambavyo naona vinajirudia, nadhani ni shida ya mtu kutoamua kupoteza muda kubuni vitu vingine vipya kwa sababu kuna prodyuza wengi upcoming yeye anajua nikishajua kupiga kiki ndio nimemamliza, hajui huu muziki ulitokea sehemu fulani na ninatakiwa kuupeleka sehemu fulani.

“Mimi kuna kipindi nilitoa hit nyingi sana nikawa najifunza vitu vingi, nikawa natembea mikoani najifunza vitu vingi sana. Sisi tuko mjini hapa hatujui huko mkoani watu wanahitaji vitu gani , unaenda kule unakutana na muziki wa tofauti kabisa, wakijaribu kujichanganya na kujua watu wanataka nini tunaweza tukafika mbali zaidi,” ameiambia Show ya XXL na kuongeza.

“Leo tunawasikia Nigeria wanajivunia muziki wao wa asili lakini wameukuza na kuwa muziki wa kisasa na wansonga mbele, lakini sisi tunashindwa kujiongeza. Lakini wapo maprodyuza ambao nawapenda wanafanya vizuri sana, kwa mfano wakina Mesen Selecta, lakini nae ana mapungufu yake ya kushindwa kubadiika lakini yupo safi sana,” amesema Manecky.

By Peter Akaro

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments