Michezo

Messi afikisha hat tricks nane michuano ya UEFA,Ipi bora kati ya hizi ?

Messi afikisha hat tricks nane michuano ya UEFA,Ipi bora kati ya hizi ?

Mchezaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, Baada ya kufungua magoli matatu dhidi ya PSV katika michuano ya UEFA Champions League siku ya Jumanne ya tarehe 18–2018, sasa amefikisha jumla ya hat tricks nane katika michuano hiyo. akiwa amefunga magoli mengi zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika michuano hiyo mikubwa kabisa barani Ulaya.

Licha ya kufunga hat tricks nane lakini amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 63 katika hizo hat tricks nane,akifuatiwa na mchezaji wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno.

Je unahisi katika hat tricks hizo nane kwa upande wako ipi ilikuwa bora zaidi kwa upande wako ?

8) APOEL 0-4 Barcelona — Nov. 25, 2014

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa michuano hii mnamo mwaka 2014 kwa kutumia mguu wake wa kushoto aliweza kuwaweka Apoel katika mazingira magumu baada ya kufunga magoli matatu akipata msaada mkubwa kutoka kwa Rafinha,Pardo pamoja na Pedro.wakati huo Barcelona wakiwa ugenini nchini Ugriki.

7) Viktoria Plzen 0-4 Barcelona — Nov. 1, 2011

Messi alifungua mlango wa magoli kwa kupata mkwaju wa penalti na kufungua ukurasa wa mabao huko Plzen, Bao la pili la Barca pia lilikuja kupitia Messi wakati alicheza kwa ushirikiano  mvizuri na Adriano kabla ya Cesc Fabregas kuongeza bao la tatu la Barca kabla ya Messi kukamilika na kufunga ubao wa magoli.

GLASGOW, SCOTLAND – NOVEMBER 23: Lionel Messi of Barcelona celebrates scoring his sides first goal during the UEFA Champions League Group C match between Celtic FC and FC Barcelona at Celtic Park Stadium on November 23, 2016 in Glasgow, Scotland. (Photo by Ian MacNicol/Getty Images)

6) Barcelona 7-0 Celtic — Sept. 13, 2016

Wakiwa Nou Camp Celtics hawatakuja kuusahau uwanja huu kamwe kupitia vijana watatu wa Kiamerika Messi,Neymar pamoja na Suarez waliweza kuwagaragaza vajana hao kutoka Scotland jumla ya magoli 7 huku Messi akiondoka na mpira siku hiyo,Messi alianza kufungua ukurasa wa magoli kabla ya Neymar kuongeza la pili lakini baada ya hapo Neymar na Iniesta waliongeza magoli mengine kablya ya Messi kufunga goli la tano na magoli ya mwisho yakipatikana kupitia messi na Suarez.

5) Barcelona 4-0 Manchester City — Oct. 19, 2016

Kwa mara ya kwanza Pep Guardiola alirudi Camp Nou kwa njia tofauti,lakini Messi alimkaribisha vizuri kwani siku hiyo aliweza kuondoka na mpira katika uwanja wa Nou Camp mbele ya kocha wake wa zamani.

4) Barcelona 4-0 Ajax — Sept. 18, 2013

Ulikuwa ni mchezo mgumu sana kwa upande mwingine ni moja ya timu ngumu kufunga magoli matatu lakini Messi alianza na mpira wa faulu kufungua ukurasa wa magoli,Messi amekuwa na mwiba kwa timu nyingi sana wanazokutana nazo.

3) Barcelona 4-0 PSV Eindhoven — Sept. 18, 2018

2) Barcelona 7-1 Bayer Leverkusen — March 7, 2012

1) Barcelona 4-1 Arsenal — April 6, 2010.

Je unahisi ni hat trick ipi unaiona ni bora kwa upande wako kati ya michezo yote hiyo nane ambayo Messi alifanikiwa kufunga zaidi ya goli mbili katika mchezo mmoja.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents