Michezo

Messi akutana na kikwazo kingine Palestina, FIFA yashusha rungu lake

Messi akutana na kikwazo kingine Palestina, FIFA yashusha rungu lake

Shirikisho la soka Duniani FIFA limemfungia miezi 12 sawa na mwaka mmoja rais wa chama cha soka Palestina Jibril Rajoub kutojihusisha na masuala ya soka kwa kile kinachosemekana kuagiza kuchomwa moto jezi za mwanasoka bora duniani kwa nyakati tano tofauti Lionel Messi.

Kupitia kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo imetoa tamko hilo linalomuhusu rais huyo wa chama cha soka Palestina,licha ya kufungiwa lakini pia anatakiwa kutoa faini ya Euro 15825 kwa kukiuka kanuni za FIFA.

Mapema mwezi june mwaka huu rais huyo aliliandika barua shirikisho la soka nchini Argentina kuwa siku wanakuja kucheza na Israel wasimchezeshe kapteni wao Messi katika mchezo wao wa kirafiki wa Argentina dhidi ya Israel  na aliongeza ” Endapo mchezaji huyo atacheza basi atawaagiza raia wa Palestina wazisake jezi za Messi nchi nzima na kuzichoma moto”

Bwana Rajoub alitoa angalizo hilo kuwa mchezo huo kati ya Argentina na Israel utakuwa wa kisiasa zaidi kwani utachezewa katika mji wa Jerusalem sehemu ambayo sio sahihi timu hiyo ya Israel kucheza katika ardhi ya Jerusalem.

Baada ya kutoa kauli hiyo hapakuwa na ulazima wa mchezo huo kuwepo na mwishowe mchezo huo ikabidi uhairishwe kwa kuhofiwa usalama wa wachezaji na mchezo huo kutupiliwa mbali.

Lakini Bwana Rajoub hakukaa kimya kwani baada ya mchezo huo kuahirishwa aliwashukuru wachezaji wa Argentina na kusema hayo ndio maamuzi sahihi waliyoyachukua kwani ni sawa na mchezaji kupewa kadi nyekundu uwanjani wakati mchezo unaendelea.

Lionel Messi amekuwa ni mchezaji anayekutana na vikwazo vingi sana kwani kipindi cha nyuma wakati ameenda kutembelea nchi ya Misri alipotoa zawadi ya viatu vyake wakati anafanya mahojiano na kituo cha MBC’s Mona El-Sharkawy.rais wa chama cha soka Misri  aliamua kuvirudisha viatu vyake kwa kudai kuwa mchezaji huyo amewadharau kwa kutoa zawadi ya viatu kwani kwa mataifa ya kiarabu kutoa viatu ni kitendo kisichokubalika kabisa.lakini pia alipotembelea nchini Gabon mwaka 2015 alishtumiwa kulidharau taifa hilo kwa kutembelea taifa hilo huku akiwa amevalia bukta lakini pia kutemtembelea rais mwenye mfumo wa kidkteta rais wa nchi hiyo Ali Bongo.

 

By Ally Juma.

 

Related Articles

3 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents